Sunday 11 August 2013

VIONGOZI WA HABATI GROUP

Viongozi hawa wamechaguliwa kwa mara ya pili baada ya kugawana Groups mbili.  Sababu ya kufanya uchaguzi tena ni kuwa wanachama walifika 46 hivyo ilibidi wanachama watengwe katika vikundi viwili, hivyo kikundi cha JUHUDI kiliundwa tena na wanachama wa mwanzo kumi na saba (17) ambapo kikundi cha BAHATI kilipunguzwa wanachama sita (6) na kupewa JUHUDI, na kuzaliwa kikundi cha pili ambacho ni BAHATI hivyo wanachama 23 kila upande waliunda vikundi.  Na hawa ni viongozi wa BAHATI Group;

MWENYEKITI
Bi. Magret Katundu

KATIBU
Bi. Alice Magesa

MWEKA HAZINA
Bi. Edna G. Robert

WASHIKA FUNGUO
Bi. Magdalena Shirima
Bi. Beatrice Kilimo
Bi. Fatuma Mtengula

WAHESABU FEDHA
Bi. Imakulata Onyango
Bi. Anitha Bana

WATUNZA NIDHAMU
Bi. Salome Chimbyangu
Bi. Donata Kindole

MAJINA YA WANAKIKUNDI BAADA YA KUTOKA VIKUNDI VIWILI JUHUDI NA BAHATI

NA HAYA NDIO MAJINA YA BAHATI GROUP

KUNDI LA I

1.   BI. EDNA G. ROBERT
2.   BI. ALICE MAGESA
3.   BI. BEATRICE KILIMO
4.   BI. CATHERINE KIRENGA
5.   BI. NICE MSHANA

KUNDI LA II

6.   BI. ANITHA BANA
7.   BI. MAGRETH C. KITUNDU
8.   BI. DONATHA KINDOLE
9.   BI. FATUMA MTENGULA
10. BW. JUMA MPIMBITA

KUNDI LA III

11. BW. JUMA MASHAKA
12. BI. IMAKULATA ONYANGO
13. BI. ELIZABETH CHRISTIAN
14. BW. ROBERT J. KADALLAH
15. BI. MAGDALENA SHIRIMA

KUNDI LA IV

16. BI. ANTIA RWEGASIRA
17. BI. SALOME CHIMBYANGU
18. BI. MARY TUNZO
19. BI. HINDU SENYANGE
20. BW. ROBERT  B. MUJUNI

KUNDI LA V

21. BW. HUSSEIN MOHAMED
22. BI. PHOIBE MSHANA
23. BW. MUTALEMWA T. MUJUNI

Monday 5 August 2013

PESCODE PICTURES AND EVENTS






















UPIMAJI WA KISUKARI KWA WANAKIKUNDI

Kutokana na mfumo wa maisha tunayoishi kwa sasa wanadamu, magonjwa yamezidi hasa kisukari.  Kikundi cha Bahati kimeona ni vyema kwa sana kwa wanakikundi kuanza kupima kipimo cha sukari.  Na imeshauriwa kila mwanakikundi alete watu wasiopungua 10 ili wapate huduma ya vipimo.

Sunday 4 August 2013

SIRI YA UTAJIRI



Siri moja wapo ya kuwa tajiri ni kujenga tabia ya kuweka akiba. Kwa wajasiriamali wadogo swala la kuweka pesa zao benki na kukopa huwa ni swala gumu hasa vijijini ambako hakuna huduma hiyo, kuna njia nyingine ambayo wataalamu wamebuni kuwawezesha kuitumia nayo ni  kuweka akiba zao kwenye VICOBA. Watu wengi wamekuwa wakijiuliza vicoba ni nini? Leo nitaelezea kuhusu historia ya mfumo wa VICOBA muundo, kanuni na taratibu za mfumo wa kuweka na kukopa vijijini  (Village Community Banks - VICOBA)


 Mfumo wa Kuweka na Kukopa Vijijini (Village Community Banks - VICOBA) ni mpya hapa nchini kwetu, mfumo huu uliingizwa nchini na Shirika la CARE International, Tanzania mwaka 2000. VICOBA imeenea katika sehemu nyingi Tanzania na idadi ya Wanachama wa VICOBA Tanzania inakadiriwa kuwa 25,542, hisa 25,542 zenye thamani ya Tshs. 2,298,780,000  vikundi 912 wastani wa wanachama 28 kila kikundi. Mikopo iliyotolewa ni Tshs. 3,065,040,000. Mfumo huu humilikiwa na wanachama wenyewe kwa njia ya kujitolea, kujenga uwezo wa mtaji, kubuni miradi ya kifamilia, kutumia vizuri mikopo. Mfumo huu ni rahisi kuendesha kwani unatumia kumbu kumbu rahisi kwa mazingira ya wanachama.  Huwawezesha wanachama kuweka akiba na kukopeshana bila kuomba msaada kwa wafadhili wala kukopa benki. Faida inayopatikana hugawiwa kwa wanachama kutokana na mchango wa kila mwanachama.  Mfumo wa VICOBA ni shirikishi unaojengwa katika msingi ya upendo, ushirikiano na kuaminiana miongoni mwa wanachama. Kutokana na sharti hili muhimu, mfumo huu unachangia kurekebisha  watu wenye tabia mbaya na wasiokubalika katika jamii na kuwafanya wawe raia wema, ili wakubalike kwenye vikundi na kudhaminiwa na wenzao. Mfumo huu unalenga katika kubadilisha taratibu mbaya (zisizoendelevu) za maisha ili kuziwezesha familia  kujiewekea malengo maalumu ya maisha na kuandaa na kuitekeleza mikakati ya kuyafikia malengo yao hatua kwa hatua. Hii ni pamoja na kuwa na matumizi mazuri ya fedha kutika familia, kujituma katika kufanya kazi.  Mfumo huu unaurahisi wa kupata mikopo ya masharti nafuu kijijini na husaidia kuwawezesha wanakijiji (wanachama) kujiwekea hisa kila wiki katika benki yao katika eneo husika na kwa kiwango kidogo kulingana na uwezo wao pasipo na gharama yoyote.

Huduma  zifuatazo hutolewa na Vicoba kama vile; uundaji wa Vikundi vya Kuweka na Kukopa Vijijini (VICOBA) kibenki kwa kujitolea, kuandaa vifaa vya kibenki na masomo ya kufundishia, kutoa mafunzo ya  uongozi wa vikundi na kuweka na kukopa. Kutoa mafunzo ya biashara yanayolenga katika kuwawezesha wanachama kuweza kuchagua miradi mizuri ya kiuchumi,teknolojia nyepesi, kuandaa mipango mizuri ya kuanzisha na kuendesha miradi yao na mbinu za kusimamaia miradi hiyo kwa faida. Kufanya utafiti wa masoko na kuandaa mikakati ya masoko, Kuendesha shughuli za kibenki na ushauri mkwa vikundi. Kusaidia vikundi kuratibu usambazaji wa pembejeo na raslimali zingine.

Muundo wa uongozi kikundi cha VICOBA huundwa na wajumbe tisa ambao huchaguliwa kidemokrasia kwa kuzingatia kazi za kila kiongozi na uwezo walionao. Miongoni mwa viongozi hawa ni: wajumbe watano wa Kamati Tendaji yaani Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina, na wahesabuji fedha wawili. Kundi la pili ni la viongozi wa kikundi ni: washika funguo za sanduku la kikundi watatu na mtunza nidhamu wa kikundi. Viongozi hawa huchaguliwa kidemokrasia na wanachama wote kwa kuzingatia sifa walizonazo katika kuongoza kikundi. Viongozi hawa hubaki madarakani kwa mzunguko mmoja ambapo sawa na miezi 9 - au zaidi Mzunguko wa kikundi hufungwa kwa muda wa wiki moja (1) hadi tatu (3), mara nyingi hii, hufanywa wakati wa sherehe za kidini au za mwisho wa mwaka au wakati wa kazi nyingi za kilimo, ukame, au uhaba mkubwa wa chakula, maji nk. Hisa zote zinazopatikana hugawanywa kwa wanachama pamoja na faida ili kusaidia kulipia gharama mbalimbali za familia kama vile kilimo, kununua chakula, nguo, ada za shule za watoto, na kugharamia sherehe na matumizi mengine muhimu ya familia. Mzunguko hufungwa ili kutoa nafasi ya kutosha kwa wanachama kushiriki kikamilifu katika kutatua matatizo yanayozikabili familia zao kipindi hicho. Mzunguko mpya huanza mara ya muda uliopangwa kupumzika kwisha. Marekebisho mhimu ya sheria za kikundi, uongozi na taratibu za kuendesha mikutano ni muhimu kufanyika wakati wa kufunga mzunguko ili kuboresha ufanisi wa kikundi katika mzunguko unaofuata.
 
Shughuli zote za vikundi vya VICOBA huendeshwa na wanavikundi wenyewe kwa njia ya kujitolea. Uzoefu unaonyesha kuwa wanavikundi huweza kuendesha vizuri shughuli zao baada ya kupatiwa mafunzo haya ya uongozi na usimamizi wa kazi za vikundi kutoka kwa wataalamu wa mfumo wa VICOBA. Kazi/wajibu wa wanakikundi ni: - Kushiriki kwenye mikutano na mafunzo ya vikundi. - Kuweka hisa za kila wiki. - Kuendesha miradi ya kiuchumi. - Kuchukua mikopo na kurejesha. - Kuchangia mfuko wa jamii na bima ya mikopo. - Kushiriki kikamilifu katika kuendesha miradi ya pamoja ya kikundi Vikundi vya VICOBA huandaa mipango yao na kufanya maamuzi yote kwa njia ya vikao ; ambavyo ni mkutano wa kila wiki , Mkutano Mkuu maalumu na Mkutano Mkuu wa kawaida wa mwaka.

Kwa sasa vikundi hivi huendesha shughuli zao chini ya sheria ya sekta isiyo rasmi na kuendesha shughuli zake chini ya uangalizi/ ulezi wa serikali za mitaa au halmashauri za miji na wilaya husika. Vikundi vinavyofadhiliwa na mashirika hulelewa na kupatiwa msaada wa kitaalamu kupitia mashirika yao pamoja na ofisi za serikali za maeneo yao wanayohusika. Ili kuhakikisha taratibu zao zinafuatwa kikamilifu na wanachama wake ni muhimu vikundi kujitungia sheria ndogo ili kuthibiti ukiukaji wa taratibu zilizowekwa na kuhakikisha kwamba kila mmoja anawajibika ipasavyo.
 
Mafunzo ndio shughuli inayopewa kipaumbele zaidi katika mfumo huu wa VICOBA. Hii ni kwa sababu tafiti mbalimbali zilizofanyika zinaonyesha kuwa kukosekana kwa ujuzi au mbinu za kibiashara ndio kiini cha matatizo yanayozorotosha jitihada za kuleta maendeleo endelevu nchini hususani kwa wananchi waishio vijijini.

Mafunzo ya mfumo wa VICOBA yamegawanyika katika makundi makubwa matatu ambayo ni:- (a) Mafunzo ya uongozi wa kikundi na uendeshaji wa shughuli za kuweka na kukopa (b) Mafunzo ya mbinu za biashara ya  kuchagua, kupanga na kusimamia mradi wa ki-uchumi (c) Mafunzo ya teknolojia rahisi za kuboresha ujuzi wa uzalishaji wa bidhaa za wana-kikundi kama vile ufugaji wa nyuki, (Bee keeping) kilimo bora cha mbogamboga kazi za mikono, ufugaji kuku, mbuzi ng’ombe, kuuza mayai, kuchimba kisima cha maji, biashara ya usafirishaji,n.k Mafunzo haya hutolewa kabla ya wanachama wa kikundi kuchukua mkopo. Lengo la mafunzo haya ni kuwaandaa wana-kikundi kiujuzi na kuwawezesha, kubuni, miradi mizuri ya kiuchumi na kuandaa mipango ya namna nzuri ya kuendesha na kusimamia biashara hizo. Mafunzo ya Kuweka na Kukopa na yale ya mbinu za biashara hutolewa kwa kipindi 12 kila wiki wanakikundi hufundishwa kipindi kimoja. Wakati huu wa mafunzo pia huweka akiba zao kwa njia ya hisa ili kutunisha mfuko wao ambao baadaye hutumika kwa kukopeshana. Mafunzo ya teknolojia rahisi hutolewa kwa wana-kikundi wanaoiendesha miradi ya uzalishaji bidhaa mbalimbali kama vile kazi za mikono, ufugaji, kilimo cha mbogamboga na shughuli zingine zinazohitaji ubunifu na mafunzo maalumu. Mafunzo haya hutolewa ili kuongeza ubora wa bidhaa zinazozalishwa Uchangiaji wa gharama za mafunzo Kwa kawaida wanachama wa VICOBA hufundishwa mafunzo wanayotaka wao wenyewe. Vikundi vimeanzishiwa mfuko wa mafunzo ambao kila mwanachama huchangia kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kuchangia gharama za mafunzo haya. Kutokana na uwezo mdogo wa wanavikundi, wafadhili mbalimbali ikiwemo Serikali na Mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakijitokeza kuchangia gharama ya mafunzo haya. Mfano Mashirika ya CARE Tanzania, WCRP, WCST, WWF, Ofisi ya Makamu wa Rais, WWF Tanzania, ITECO Engineering, Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Uropean Union, shirika lisilo la kiserikali la LAMP, Orgut, FREBU CO. LTD, nk
 
Kulingana sheria mama za mfumo huu wa VICOBA, mwanachama anatakiwa kuweka hisa 1-3 kila wiki. Kiwango cha hisa huamuliwa na wanakikundi wenyewe. Hata hivyo, kulingana na thamani ya fedha yetu kiwango cha chini kinachoweza kumnufaisha mwanachama kwa sasa ni shilingi mia tano (500). Mwanachama anaruhusiwa kuweka hisa moja, mbili hadi tatu kila wiki ili kutunisha mfuko. Matumizi ya Hisa ya mwanachama Hisa ni muhimu zana kwa mwanachma kwa sababu zifuatazo: (i) Ni akiba ya mwanachama ambayo huichukua mwishoni mwa mzunguko pamoja na faida au wakati mwingine wowote apatapo matatizo kulingana sheria za kikundi chao. Kwa kawaida hisa zinazochukuliwa katikati ya mzunguko hutolewa bila faida (ii) Hisa hutumika kama kigezo cha kujua kiwango cha mkopo ambacho mwanachama wa kikundi anaweza kuomba kutoka  

kwenye benki yao. Mfumo wa VICOBA unamruhusu mwanachama kuchukua mkopo hadi mara tatu ya hisa alizoweka. Hata hivyo, uamuzi wa kupatiwa mkopo huo utazingatia matumizi na uhakika wa mwanachama kumudu kurejesha kwa wakati unaotakiwa. (iii) Hisa hutumika kama dhamana ya mkopo unaotolewa kwa mwanachama wa kikundi kidogo cha watu watano. Dhamana ya awali ni ya mkopaji mwenyewe (Primary Guarantor) na dhamana ya pili ni ya wanachama wenzake wanne (4) wa kikundi kidogo (Secondary Guarantors) Hii inamaanisha kuwa ili kuhakikisha kuwa mikopo yote inayotolewa kwa wanachama 5 wa kikundi kidogo inadhaminiwa kikamilifu mambo yafuatayo yanatakiwa kuzingatiwa: (a) Wanachama wa kikundi kidogo wasiruhusiwe kuchukua mkopo wakati mmoja. Tofauti ya mwezi mmoja hadi miezi miwilli ni kipindi kizuri kwa wastani wa watu wawili wawili kila awamu (b) Kunatakiwa pawepo na makubaliano maalumu baina ya mwanachama anayekopa na wale wanaomdhamini juu ya hatua zinazoweza kuchukuliwa na wadhamini endapo mdhaminiwa hatatimiza wajibu wa kulipa deni lake kwa uzembe (c) Mwanachama anayekopa kutoka kwenye benki ya kikundi anatakiwa kuchangia mfuko wa bima ya majanga itakayokubaliwa na kikundi kwa mfano kufariki kwa mkopaji, kuugua kwa muda mrefu na kupoteza uwezo wa kufanya kazi/ kulemaa kwa mkopaji kuunguliwa au kuibiwa mali za biashara ya mkopaji, ukame, nk Taratibu za utoaji na urejeshaji wa mikopo. Mikopo inayotolewa kwa wanachama wa VICOBA unatakiwa kurejeshwa na nyongeza (Interest) ndogo ambayo hutumika kwa kutunisha mfuko wa kikundi. Nyongeza hii hugawanywa kama faida kwa wanachama kwa kuzingatia kiwango cha hisa alizoweka kila mmoja. Mikopo ya mwanzo ambayo kwa kawaida huwa midogo kuliko mikopo inayofuata hutakiwa kulipwa kwa kipindi cha miezi 3 . Lengo ni kumwezesha mkopaji aweze kulipa haraka na kuchukua mkopo mkubwa pale hisa zake zinavyopanda ambao utamwezesha kumudu kuanzisha na kuendesha biashara madhubuti zaidi Mfumo wa VICOBA unamtaka mkopaji kurejesha mkopo aliokopa mwishoni mwa kipindi cha mkopo wake kwa awamu moja. Mkopaji anatakiwa kulipa sehemu ya nyongeza inayoiva kila ifikapo wiki ya mwisho ya mwezi. Sehemu ya mwisho hulipwa pamoja na mkopo Mfano: Endapo mwanachama atakapokopeshwa shilingi 100, 000.00 kwa nyongeza ya 10% (10,000.00) kwa kipindi cha miezi mitatu atarejesha kama ifuatavyo:- Mwezi wa 1 Mwezi wa 2 Mwezi wa 3 Jumla 3,400 3,300 3,300 100,000 110,000 Endapo mkopo wa thamani hiyo hiyo (Shilingi 100,000.00) utarejeshwa kwa kipindi cha miezi sita kwa gharama (nyongeza) ya asilimia ishirini 20% (20,000.00), marejesho yatakuwa kama ifuatavyo:- Mwezi wa 1 Mwezi wa 2 Mwezi wa 3 Mwezi wa 4 Mwezi wa 5 Mwezi wa 6 Jumla 3,400 3,400 3,300 3,300 3,300 3,300 100,000 120,000 Kwa kawaida mwanachama anayemaliza kurejesha mkopo wake vizuri anaruhhusiwa kuomba mkopo mwingine mara moja ili kufidia pengo la mtaji katika biashara yake. Ufuatiliaji na Uthibiti wa shughuli za vikundi vya VICOBA Makatibu wa vikundi vya VICOBA wanatakiwa kufuatilia mwenendo wa vikundi vyao na kuandaa taarifa za kila mwezi, miezi mitatu na taarifa za kila mwaka ambazo hujadiliwa na kupitishwa na mikutano mikuu ya vikundi vyao. Afisa (Mkufunzi) anatakiwa kutoa maelekezo na msaada wa kiufundi pale inapobidi na kuwajulisha wafadhali wa vikundi na wadau wengine juu ya maendeleo ya vikundi kadiri inavyotakiwa.