Mwanachama yeyote anayejiunga kwa ridhaa yake katika kikundi chochote kile kwa manufaa yake na jamii nzima ni lazima ahudhurie kila kikao cha siku iliyopangwa na kikundi.
Ukiona mtu ana udhuru katika kikundi basi ujue huyo hajitambui na hatakuja kufanikiwa hata iweje, maana kama umeona kuna umuhimu wa kujiunga na wenzako ili muwe familia moja basi tambua huyo si familia, pia tambua kikundi ni sehemu ya kusaidiana, je utasaidiaje au kusaidiwaje ikiwa wewe udhuru kila kukicha, je kikundi kitakuwa na maendeleo gani ikiwa wewe una udhuru. Mbaya zaidi siku unayofika katika kikao unawarudisha wanakikundi nyuma maana utaanza kuhoji maswali yasiyo na msingi wakati wenzako walishapita huko.
Nashauri wanavikundi mukutane wote kila kikao kwa siku iliyopangwa itokee bahati mbaya mwanakikundi awe na safari, amefiwa, au kuumwa. Lakini kama unajitambua unaweza kutenga dakika 45 kila siku iliyopangwa ili kuhudhuria vikao.
"Wote tuna majukumu lakini kama yako yamezidi basi hufai kuwa katika kikundi"