Sunday 17 November 2013

UDHURU KATIKA VICOBA NI KUTOKUJITAMBUA

Mwanachama yeyote anayejiunga kwa ridhaa yake katika kikundi chochote kile kwa  manufaa yake na jamii nzima ni lazima ahudhurie kila kikao cha siku iliyopangwa na kikundi.
 
Ukiona mtu ana udhuru katika kikundi basi ujue huyo hajitambui na hatakuja kufanikiwa hata iweje, maana kama umeona kuna umuhimu wa kujiunga na wenzako ili muwe familia moja basi tambua huyo si familia, pia tambua kikundi ni sehemu ya kusaidiana, je utasaidiaje au kusaidiwaje ikiwa wewe udhuru kila kukicha, je kikundi kitakuwa na maendeleo gani ikiwa wewe una udhuru.  Mbaya zaidi siku unayofika katika kikao unawarudisha wanakikundi nyuma maana utaanza kuhoji maswali yasiyo na msingi wakati wenzako walishapita huko.
 
Nashauri wanavikundi mukutane wote kila kikao kwa siku iliyopangwa itokee bahati mbaya mwanakikundi awe na safari, amefiwa, au kuumwa.  Lakini kama unajitambua unaweza kutenga dakika 45 kila siku iliyopangwa ili kuhudhuria vikao.
 
"Wote tuna majukumu lakini kama yako yamezidi basi hufai kuwa katika kikundi"

Monday 11 November 2013

"Thinkers think and doers do. But until the thinkers do and the doers think, progress will be just another word in the already overburdened vocabulary of the talkers who talk."

Wanakikundi lazima tutambue kuna Thinkers na pia kuna Doers, yaani kuna wanaofikiri na wanaotenda je wewe uko upande upi?

Mfikiriaji au Mtendaji?

JINSI YA KUUNDA KIKUNDI CHA VICOBA

VICOBA (Village Community Bank) ni mfumo wa kuweka na kukopa kwa wanachama waliojiunga kwa pamoja na kuunda kikundi kwa malengo ya kujikwamua kiuchumi.

Mfumo huu ulianza Tanzania miaka kumi iliyopita na umeonyesha mafanikio makubwa kwa wanachama wake kuweza kukopeshana, kusaidiana katika matatizo mbalimbali, kuanzisha miradi ya pamoja ya kiuchumi.

MALENGO/MADHUMUNI YA KUUNDA VICOBA
Madhumuni ya kuunda vicoba ni kuunganisha nguvu na rasilimali za wanachama ili kuondoa umasikini na kuleta maendeleo kwa kufanya yafuatayo:-
  • Kuchangia/kununua hisa
  • Kuchangia mfuko wa jamii
  • Kuendesha mfuko wa kuweka na kukopa
  • Kushiriki katika mafunzo ya kuongeza ujuzi wa biashara, uongozi na uanzishaji wa shughuli mbalimbali za pamoja za maendeleo.
  • Kutafuata soko la pamoja na la uhakika kwa bidhaa za wanakikundi 

Kuna tofauti gani kati ya VICOBA na SACCOS?



VICOBA na SACCOS ni vikundi vya kiuchumi vyote vina malengo sawa isipokuwa mfumo wa uendeshaji.
  1.  Katika VICOBA wanachama uweka kiwango cha hisa na mara nyingi huanzia Sh.1000 na kuendelea, kiwango hicho ni kidogo ukilinganisha na kiwango cha hisa katika SACCOS.
  2.  WanaVICOBA umaliza mzunguko wao baada ya miezi kumi na mbili (12) na kufanya tathmini ikiwemo kugawana makusanyo na faida.
  3. Riba ya mkopo katika VICOBA ni ndogo (mara nyingi haizidi 10%)
  4. Kikundi cha VICOBA kinaundwa na wanachama 15-30, wanaoishi eneo moja au wanaofanya kazi pamoja.
  5.  Gharama za uendeshaji wa VICOBA ni ndogo kwani hakuna ofisi (wanachama huchagua mahali pa kukutana kwa muda usiozidi saa moja), vile vile viongozi wa VICOBA hawaajiriwi (wanafanya kazi za kujitolea)
VICOBA ikikuwa inaweza kuunda SACCOS. Mfumo wa Vicoba ni mzuri hasa kwa falsafa ya kuanza kidogo ili kuwa na kitu kikubwa hapo baadae. Licha ya kujihusisha na shughuri za kuweka na kukopa, wanavicoba husaidiana katika matatizo mbalimbali kama msiba na ugonjwa. Vile vile wanavicoba wanaweza kuanzisha mradi wa pamoja wa kikundi kwa kuunganisha rasirimali ndogo walizonazo. 
Hatua za Kuunda kikundi cha VICOBA
  1. Watu wenye wazo la kuanzisha kikundi kukutana (watu hao wasipungue kumi na tano na wasizidi thelathini)
  2. Wanachama kukusanya fedha za kiingilio (mara nyingi ni Sh. 10,000) kwa mwanachama. Fedha hiyo hutumika kununua vifaa kama leja,kasiki n.k. Fedha ya kiingilio vilevile hutumika kugharamia mafunzo ya awali na gharama ya usajili wa kikundi)
  3. Wanachama kuanza mafunzo yatakayosimamiwa na mwalimu mtaalamu wa mfumo huu wa vicoba.
  4. Wanachama kutunga katiba na sheria zitakayojumuisha kiwango cha hisa, mfuko wa jamii, siku ya kukutana n.k

Vicoba husajiliwa Brela kama jina la biashara (Business name) na kutambuliwa na halmashauri ya manispaa husika kupitia ofisi ya maendeleo ya jamii.
Mfumo huu ni rahisi kuuendesha na unamanufaa makubwa katika maendeleo ya kiuchumi. Ni fursa kwa vijana wenye mitaji midogo kuanzisha vikundi hivi ili kuunganisha rasirimali ndogo walizonazo na kwa pamoja kujiletea maendeleo.

Elimu ya Ujasiriamali ni Lazima kwa VICOBA

Imebainishwa kuwa vikundi vingi vya vicoba nchini licha ya kukabiliwa na changamoto ya mtaji vinahitaji elimu ya ujasiriamali ili Kuweza kufahamu jinsi ya kufanya biashara kwa faida badala ya kufanya biashara kwa mazoea jambo linalofanya vikundi vingi Kufilisika na kushindwa kuendelea.

KIKUNDI LAZIMA KIBUNI MIRADI MIKUBWA YA KATI NA MIDOGO

Kuna aina nyingi za miradi

Ipo miradi Mikubwa

Ipo miradi ya Kati

Ipo miradi Midogo

Kikundi kinatakiwa kufanya mambo haya na siku vinginevyo, la sivyo haina haja ya kuwa na kikundi

Sunday 10 November 2013

Lazima Tuelewe

wanakikundi ni lazima tuelewe wiki ya 14 hii, tujifunze kazi za mkutano mkuu unaofanyika maramoja kwa maka ambao ndio unachagua viongozi.

Tujifunze jinsi ya kutatua migigoro itakapojitokeza

Tujifunze jinsi ya kuweka akiba

Jinsi ya kusimamia mikopo ya wanachama

Tujifunze jinsi ya namna ya kutunga kanuni na taratibu za vikundi na kuandika michanganuo rahisi ya biashara, ambayo ni msaada mkubwa katika kupanua wigo wa biashara zetu.

Kimsingi hatutakiwi kuvunja kikundi mwisho wa mwaka bali tuanzishe miradi ya vikundi ambayo itashirikisha wanachama wote.

Lazima kikundi chetu kitambulike serikali za mtaa pamoja na majirani

Lengo linguine ni kupeleka ujumbe kwa wananchi kwamba VICOBA kama wengine wanavyodhani kimakosa kuwa ni vikundi vya kufa na kuzikana.  Wananchi wanakumbushwa kwamba hivi ni vikundi vya maendeleo ya uchumi.

Pia tujipange kualika vikundi mia tatu kuzindua kundi letu la BAHATI VICOBA
 hapa tutapata kiasi cha shilingi milioni tisa (9,000,000/=) za kuzindilia kikundi


BAHATI VICOBA kina bahati kama jina lake, kuna THINKERS ila kuna watu wanataka kuharibu kundi kama tutaendelea kupanga mikakati ya kibwege nje ya mikutano na kulalama nje ya vikao halali kundi hili litakuwa HOPELESS na hakuna maendeleo yatakayofikiwa.  wanajulikana waharibifu wa kikundi ila ipo siku watatajwa na wataachiwa kundi na wenye akili watatoka

VICOBA SI VIKUNDI VYA KUSAIDIANA WAKATI WA KUFA AU KUUMWA

VICOBA ni

BONYEZA HAPA:

http://www.habarileo.co.tz/index.php/makala/15221-vicoba-si-vikundi-vya-kufa-na-kuzikana-bali-vya-kiuchumi

VIONGOZI WA BAHATI VICOBA

MWENYEKITI
Saidi CHIMBIYANGU

KATIBU
Justine MADATI

MTUNZA HAZINA
Edna ROBERT

WAHESABU FEDHA
Robert MUJUNI
Anita BANA

WASHIKA FUNGUO
Fatuma MTENGULA
Mama BONGE
Mama NYALUSI

MTUNZA NIDHAMU
Mama CHIMBIYANGU


BIASHARA

Mchele:
Justine MADATI

Viti:
Juma MPIMBITA

MAKUSANYO YA FEDHA ZA VITI
Dada MLELWA

SUKARI
Justice MADATI

Biashara ya Mbogamboga



Biashara ya Upambaji



Biashara ya Mayai ya Kuku wa Kienyeji kwa Kikundi cha BAHATI VICOBA

BAHATI VICOBA UFUGAJI






Tunashauriwa kuwa na biashara ya ufugaji wa Mbuzi, Kuku na Ng'ombe pia uuzaji wa mayai

SIFA ZA KIONGOZI BORA

Kisaikolijia sifa za kiongozi ziko wazi na ni muhimu, mtu kuwa nazo kabla au baada ya kupewa cheo. Leo tunataka kuziangalia kwa undani sifa hizi, ili kama wananchi au viongozi wenye dhamana ya kuchagua watu wa kuongoza tuwatazame watu kwa sifa zao kabla na baada ya kuwapa nafasi. Sifa za kiongozi ni hizi zifuatazo:

 1. Awaze mafanikio makubwa
Kiongozi bora lazima awe na maono ya juu ya kuhakikisha kuwa nchi yake, kampuni yake sekta yake inapata mafanikio makubwa, hii ndiyo itakuwa dira ya kazi yake itakayompa muongozo wa kusimamia wafanyakazi na watendaji wote walio chini yake kufikia kiwango cha mafanikio anachokiwaza. Kiongozi asiyekuwa na mawazo ya juu ya kuendelea kutoka mahali alipo hafai.

 2. Awe na nia
Haitoshi kwa kiongozi kuwa na mawazo chanya peke yake bila kuwa na nia ya kuyatimiza. Hivyo, kiongozi atafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi endapo tu atakuwa na uwezo wa kuratibu vema na kutekeleza alichowaza. Ajue njia anayopita, awatangulie anaowaongoza kwa vitendo.

 3. Ajitambue mwenyewe
Lazima kiongozi ajitambue mwenyewe ni mtu wa namna gani, ajue uwezo wake na upungufu wake na awe tayari kujiongezea maarifa kila siku, ili aweze kukabili changamoto na mabadiliko ya ulimwengu. Asome, afuatilie mambo yanavyokwenda na ajifunze kwa wenzake kuhusu kufanikisha malengo yake.

 4. Asimamie maamuzi
Kuna wakati malengo hukumbana na vikwazo, hivyo ni wajibu wa kiongozi kusimamia maamuzi sahihi na kuwa mtu wa mwisho. Kiongozi mwenye kubadilika badilika kama kinyonga, hafai kwa vile kukosa msimamo kuna maanisha udhaifu wa mipango na kujiamini.

 5. Adhibiti msongo wa mawazo
Tunamtarajia kiongozi mzuri awe ni mtu mwenye kupunguza msongo wa mawazo, ili kuifanya akili yake ifikie maamuzi sahihi, lakini kama atakuwa mwenye kuwaza mengi, atajikuta anachanganyikiwa na kuwa mtu wa jazba katika maamuzi na hivyo kuipotosha jamii.

 6. Akubali kukosolewa
Viongozi wasiokuwa na sifa za uongozi huwa hawakubali kukosolewa, wakidhani kuwa hiyo ndiyo njia ya kuthibitisha msimamo wao na usahihi wao. Kiongozi makini ni yule ambaye atakuwa tayari kukosolewa na kuwapongeza wanaomkosoa kwa kutazama mwenendo wake na usahihi wake. Asiyekubali kukosolewa hafai kuwa kiongozi.

 7. Awe msikilizaji
Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kuwasilikiza watu walio chini yake, apokee maoni yao na ikiwezekana ayafanyie kazi. Lakini pia anatakiwa kuwafahamu kwa undani, ili aweze kuwaongoza vema kufuatana na hali zao. Akiwa na watu walemavu wenye kasoro kadhaa wa kadhaa anatakiwa kuwatambua kabla na baada ya kuwa kiongozi wao. Kuongoza usichokifahamu ni ujinga.

 8. Afuate haki
Kiongozi imara anatakiwa kufuata haki katika kuongoza kwake, asijione mwenye haki zaidi ya wale anaowaongoza katika sheria. Ni muhimu kwake kuwafanya walio chini yake kujiona wako huru katika mawazo na matendo. Kiongozi anayetumia nguvu na ukali kuongoza watu hafai. Hata yule mwenye kujivunia uongozi wake naye hafai.

 9. Awe egemeo la watu
Sifa nyingine ya kiongozi ni kuwa egemeo la watu wake katika shida na raha. Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kusikitika, kuomboleza, kufurahi pamoja na watu wa chini yake bila kujitenga nao. Ajitolee kuwatumikia watu kwa hali na mali na awe tayari kutumika zaidi kwa maslahi ya wengine.

 10. Atie moyo watu
Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuwatia moyo walio chini yake ili waweze kuendeleza vipaji vyao. Haipendezi kwa kiongozi kuwavunja moyo watu kwa kauli za kudharau kazi na jitihada zao walizojaribu kufanya katika kutekeleza majukumu yao kama wafanyakazi au wananchi.

 11. Afurahie mafanikio
Sifa nyingine muhimu ya kiongozi ni kuwa tayari kufurahia mafanikio aliyopata pamoja na watu wake. Ni wajibu wa kiongozi kutoa tuzo, kuwashukuru wafanyakazi wake na kuwa tayari kuwapa ofa. Hii itasaidia kuwafanya watu waone hawajapoteza nguvu zao katika utendaji wao na kwamba wanakubalika. Si busara wakati mwingine kuwakosoa watu mbele ya hadhara na kueleza kutofurahishwa na kazi zao.

 12. Aungane na wa chini yake
Mtu kuwa kiongozi haimaanishi amekuwa wa tofauti na watu wengine kiasi cha kushindwa kuchangamana nao kama wanavyofanya baadhi ya viongozi. Kiongozi mwema ni yule atakayeungana na watu wake katika maisha ya kawaida. Kuwa kiongozi haimaanishi kwamba watu watakufuata wewe kila siku, wakati mwingine wewe unatakiwa kuwafuata wao na kuwa nyuma yao hata mahali walipokosea au wanapokabiliwa na makosa, watetee na uoneshe kuwajali na kuwapigania, makosa utayahesabu baada ya utetezi wako kukamilika.

13. Akubali lawama
Kama kiongozi amefanya mambo ambayo jamii haikupendezwa nayo anachotakiwa kufanya ni kukubali kulaumiwa. Ikiwa anaongoza kitego cha umeme kwa mfano na watu hawakupata nishati hiyo kwa wakati hatakiwi kukwepa lawama, vivyo hivyo kwenye wizara na idara au nchi kwa ujumla.

14. Afahamu kutatua matatizo
Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuzuia migogoro na kuitatua kwa haraka. Muongozo mzuri katika eneo hili umesimama katika mawasiliano na watu wa chini, mawasiliano haya ndiyo yatakayomuwezesha kiongozi kujua matatizo waliyonayo wafanyakazi wake au hata jamii anayoiongoza na hivyo kumfanya apate wasaa wa kuyashughulikia mapema.

 15. Ajifunze kwa makosa
Wakati mwingine mawazo na mipango inaweza ikaenda kombo, hivyo ni wajibu wa kiongozi kujifunza kutokana na makosa yake au ya wale anaowaongoza, ili kuepuka kurudia makosa yale yale na kumfanya apoteze sifa za kuwa kiongozi mzuri.
Mwanafalsafa Winston Churchill aliwahi kusema "The price of greatness is responsibility." Thamani ya ukuu ni uwajibikaji.

 16. Awe mwaminifu
Miongoni mwa maeneo magumu kabisa yaliyowashinda na yanayoendelea kuwashinda viongozi wengi ni uaminifu. Kiongozi bora ni yule ambaye yuko tayari kusimamia muongozo wa katiba ya nchi au marufuku alizowekewa katika madaraka yake. Hii inakwenda sambamba na kutowaonea, kuwanyanyasa wa nchini yake kwa kutumia cheo chake.

 17. Awe mkweli
Viongozi wengi hasa wa kisiasa siku hizi ni waongo hakuna mfano, wamejaa ahadi zisizotekelezeka na hata wanapogundua kuwa hawana uwezo au wamekwama kuzitimiza, hawaoni haja ya kutubu mbele ya wanaowaongoza. Kiongozi makini ni yule atayekuwa tayari kuonesha ubora wa matendo na kauli zake.

 18. Asiwe mwenye majungu
Kuna baadhi ya viongozi kwenye maofisi wanaendekeza sana majungu na pengine kuyapa umuhimu wa hali ya juu. Hii ni sifa mbaya kwa kiongozi yo yote, hivyo anayetumikia ‘umbea’ katika ofisi aliyokabidhiwa kama mkuu anapaswa kuondolewa. Kiongozi makini atatumia uwezo wake kuzuia watu wasimsengenye/wasisengenyane kwa kuwa muwazi na mwenye kufungua milango ya watu kumuona na kumlaumu na kueleza hisia zao.

 19. Awe bora
Kwa kila analofanya kama kiongozi lazima alifanye kwa ubora, asiwe mtu mwenye kulipua kazi na kufanya chini ya kiwango cha uwezo wake. Kila siku katika kazi, maamuzi, usimamizi, utekelezaji lazima atumike zaidi ya uwezo wake.

KUTOKA KUAJIRIWA MPAKA KUJIAJIRI MAMBO 8 YA KUZINGATIA​.

Kuna sababu mbalimbali kwanini mtu atake kuajiri, badala ya kuajiriwa, mfano kipato kidogo anachopata katika kazi husika, hitaji la kutaka uhuru zaidi binafsi wa kufanya kazi, hitaji la kuweza kutoa ajira kwa wengine na zaidi sana kuweza kutumia vema kipaji na uwezo wa kuzalisha ambao katika kazi ya sasa mtu hapati nafasi ya kufanya hivyo.
Kujiajiri ni jambo linalohitaji maandalizi ya muda mrefu na kuna mambo ya msingi kuyafahamu, haiwezekani tuu , ukaacha kazi na kusema ok, acha nijiajiri.
Makala hii inachambua mambo ya msingi ya kujiandaa na kuyafahamu kabla mtu hajaamua kuacha kuajiriwa.

Mkakati ni muhimu: Wazo au ndoto isiyo na mkakati wa kuitimiza ni upuuzi yaani ndoto hiyo au wazo hilo halina maana, hivyo basi ndoto yako ya kujiajiri siku moja, ni lazima iwekewe mkakati wa kuifanikisha ikiwa ni pamoja na muda hasa wa lini utaitimiza hiyo ndoto.
Katika kuweka mkakati huu wa kutimiza ndoto yako, fanya utafiti wa kina kuhusu mipango yako binafsi ya maisha, mtazamo wako kuhusu maisha, mpenzi/mke wako, familia yako, na hali ya jamii kwa ujumla inavyoenda kama vile mabadiliko ya hali ya kisiasa, teknolojia, na uchumi.
Tengeneza malengo ya aina ya shughuli unayotaka kuifanya ukiacha kuajiriwa, na pima uwezekano wa shughuli hiyo kufanyika kweli na kama itakulipa. Utambue pia aina ya watu na rasilimali nyingine utakazozihitaji, na jinsi utakavyozipata.
Unahitaji fedha: Ndio, unahitaji kiasi cha fedha za kutosha kununua vifaa na malighafi za kutengenezea bidhaa yako. Pia unahitaji fedha za kuwalipa wafanyakazi wako, na zaidi sana , unahitaji fedha za kuendesha maisha yako na familia yako , kwa kipindi fulani kabla ya biashara kuanza kukulipa mshahara. Hivyo kabla haujaacha kibarua chako, hakikisha umetengeneza bajeti ya kutosha na una akiba ya kutimiza mahitaji ya bajeti yako. Usingependa uache kazi halafu uanze kuwa omba omba kwa rafiki na jamaa, au uanze kujuta.
Network ni muhimu: Kumbuka katika kujiajiri kwako, utahitaji wateja, washirika, wafanyakazi na hata washauri mbalimbali ili mambo yako yaende vizuri. Hivyo, wakati ukiwa umeajiriwa ndio wakati wako muafaka wa kutengeneza na kupanua wigo wako wa watu unaowafahamu na waliokaribu nawe.
Kumbuka kuendeleza mawasiliano kwani watu hawapendi kuona wewe unataka kuwatumia tuu kisha unawatupa. Endeleza mawasiliano walau hata kwa salamu tuu. Zaidi sana, heshimu watu wote, hata usiowafahamu au wale unaodhani 'sio watu muhimu'.
Jenga taswira nzuri kwa jamii kwa lugha fasaha, picha na matukio mengine, usifanye watu wakufikirie vibaya.
Usipitwe na wakati: Hakikisha kuwa unafuatilia taarifa za matukio, dili na watu wanaohusiana na aina ya shughuli unayopanga kuifanya wakati utakapojiajiri. Hii itakusaidia kupata uzoefu na kusoma alama za nyakati, na pengine kutambua fursa nyingine zaidi.
Endelea kujifunza zaidi kuhusu kazi yako, watu na jamii kwa ujumla kwani kujiajiri kunahitaji uzoefu zaidi, na zaidi sana uwezo wa kupambana na changamoto nyingi ambazo nyingine haujawahi kukutana nazo kabisa, ila taarifa za awali na kujua jinsi mambo yanavyoenda kwa ujumla katika jamii vitakufanya ushinde changamoto.
Maana halisi ya biashara: Baada ya kuacha kuajiriwa, hautarajii kuwa mtu wa ‘kuganga njaa’ yaani kufanya biashara ili mradi tuu hela iingie, lakini haujui mwelekeo wa biashara yako upoje, na wala hakuna mkakati wa kuikuza na kuimarisha biashara husika.
Biashara inahusu kutimiza mahitaji ya watu, kwahiyo ili mradi utakuwa na uwezo mkubwa wa kutimiza mahitaji ya watu, na kuendelea kuhamasisha watu zaidi kuja kwako uweze kutimiza mahitaji yao , basi biashara itakua, na itaendelea kuwa endelevu.
Kinyume cha hapo, ushindani utakutoa katika biashara kwani wateja watakambilia kwa wengine. Biashara sio tuu kupata wateja, ni vile kuweza kuendelea kupata wateja na kuendelea kupanua biashara.
Inabidi uipende shughuli husika unayoifanya, na uweze kutimiza mahitaji ya wateja kupitia biashara husika.
Muda wako mwingi utautumia katika shughuli yako mpya utakayojiajiri hivyo, kama ambavyo kazi uliyonayo pengine ‘inakuboa’, hakikisha ajira yako binafsi ‘haikuboi’.
Umuhimu wa wafanyakazi: Watendaji wa shughuli husika za biashara yako utakayoianzisha ni muhimu wawe wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha wa kufanya shughuli husika, na uweke mikakati ya kuwapatia nyenzo zote muhimu za kufanyia kazi ikiwemo teknolojia na mazingira mazuri ya kazi. Hivyo basi wakati unajiandaa kujiajiri tilia maanani hili katika bajeti yako ya kuajiri. Usingependa wafanyakazi wao wajisikie vibaya kama vile wewe ulivyojisikia vibaya katika ajira yako fulani (pengine ajira yako ya sasa). Muda huu ambao umeajiriwa, ndio muda pia muafaka wa kusaka 'vipaji'- yaani watu ambao utafanya nao kazi utakapojiajiri.
Inakuhusu wewe : Mafanikio yako katika kujiajiri yanategemea mambo mengi ila zaidi sana yanakutegemea wewe. Je, nini hasa sababu yako ya kutaka kujiajiri?
Ni kweli una bidhaa au huduma haswa ya kupeleka sokoni itakayokufanya iendeshe maisha yako na kuiendeleza biashara husika au ni hasira tuu za jinsi bosi wako anavyokuchulia hapo ofisini kwako, au kwakuwa mshahara uliopo sasa haukutoshi. Je, mipango yako mingine ya maisha ipoje?
Ndoto zako za kusoma, au kuishi sehemu tofauti tofauti, pengine mkoa mwingine tofauti na uliopo sasa, au pengine hata nchi husika. Je, yote hayo yanaathiri vipi mipango na mikakati yako ya kujiajiri, bila kusahau msukumo toka kwa familia yako.
Ndoto sahihi: Ni kweli kuwa upo sahihi kufikiria au kuota kufanya biashara kubwa na yenye mafanikio sana, lakini kumbuka mafanikio hayaji kwa usiku mmoja, na hata kama yatakuja kwa usiku mmoja, inahitajika kazi ya muda mrefu kuyafanya yawe endelevu.
Hivyo basi, usingoje wakati ‘muafaka’ wa wewe kuwa na kiasi kikubwa cha fedha au kwamba ‘umeyaset’ vema mambo yote.
Anza kidogo kidogo, kubali kufanya makosa, na tambua kuwa hata kama utafanya uchambuzi na uchunguzi wa kutosha kuhusu soko, jamii na teknolojia, hali halisi unayoenda kukumbana nayo inaweza kuwa tofauti na ile uliyojifunza wakati wa uchambuzi au uchunguzi wako kwakuwa hicho unachoenda kufanya ni kipya hakikufanyiwa uchambuzi, bali unakifanya kutokana na uchambuzi uliofanya hapo awali.
Kuna mtu mwingine atakuja kutumia makosa au mafanikio yako kupanga mambo yake.

Hadi sasa BAHATI VICOBA imekopesha zaidi ya shilingi milioni nne (4,000,000/=)

Ndugu wanakikundi,

Tunafuraha kuwatangazia kuwa hadi sasa wiki ya 14 kikund chetu kimeanza kukopeshana na hadi sasa kikundi kimetoa mkopo wa shilingi milioni nne taslimu.

Umbeya, majungu, Kusengenya vinavuruga maendeleo

Wanakikundi wa Bahati VICOBA mnaaswa kuwa na ushirikiano na upendo katika kikundi chenu kama hamtaifuata salamu ya VICOBA basi mtabaki kunung'unika na kusengenya pembeni.  Wengi wenu hamna kazi za kufanya hivyo inawafanya kila muambiwalo la msingi mnahisi kuburuzwa ila tulizeni akili na mjue hamburuzwi ila hakuna maendeleo ya lelemama, kubalini fauateni maelekezo mnayopewa na wabunifu ili muje muone maendeleo.

Ndugu wanakikundi nayaongea haya kwa uchungu kwa kuwa naona kuna watu wasio waaminifu wanaanza kuvuruga kikundi, hakuna ubunifu, kuna majungu tu, kila tunalopanga mnalipeleka kwenye kundi linguine ni aibu sana mwanakikundi kunyenyekea kundi linguine kisa unapewa HISA na JAMII ni aibu sana kufuatilia fedha iliyo benki kama vile imeliwa hamtaendelea nawaambia.  Kama mnataka maendeleo fuateni mambo ya msingi na myafanyie kazi na si kukaa pembeni na kuanza kusimanga.