Sunday 4 August 2013

LENGO NA SHUGHULI ZA KIKUNDI





          Lengo na shughuli za kikundi chetu cha BAHATI ni kuinua     hali ya maisha  

  ya wanachama na familia zao.

          Ili kufika lengo la kikundi wanachama wa kikundi chetu watatekeleza shughuli zifuatazo

          Kushiriki kwenye mafunzo ya kujenga uwezo

·         Mafunzo ya uongozi na taratibu za kuendesha benki kikundi

·         Mafunzo ya biashara (SPM)

·         Mafunzo ya Teknolojia rahisi

·         Mafunzo mengineyo

          Kuendesha benki ya kikundi ili kuwawezesha wanachama kujiwekea akiba (hisa) na kuchukua

                Mikopo yenye masharti nafuu.

          Wanachama kuendesha miradi endelevu ya kiuchumi pamoja na wanafamilia wao ili kuongeza

                 Kipato cha familia

         Wanachama kusaidiana kuendesha mradi wa pamoja kwa lengo la kutoa huduma muhimu kwa   jamii na kujipatia kipato

No comments:

Post a Comment