Sunday 17 November 2013

UDHURU KATIKA VICOBA NI KUTOKUJITAMBUA

Mwanachama yeyote anayejiunga kwa ridhaa yake katika kikundi chochote kile kwa  manufaa yake na jamii nzima ni lazima ahudhurie kila kikao cha siku iliyopangwa na kikundi.
 
Ukiona mtu ana udhuru katika kikundi basi ujue huyo hajitambui na hatakuja kufanikiwa hata iweje, maana kama umeona kuna umuhimu wa kujiunga na wenzako ili muwe familia moja basi tambua huyo si familia, pia tambua kikundi ni sehemu ya kusaidiana, je utasaidiaje au kusaidiwaje ikiwa wewe udhuru kila kukicha, je kikundi kitakuwa na maendeleo gani ikiwa wewe una udhuru.  Mbaya zaidi siku unayofika katika kikao unawarudisha wanakikundi nyuma maana utaanza kuhoji maswali yasiyo na msingi wakati wenzako walishapita huko.
 
Nashauri wanavikundi mukutane wote kila kikao kwa siku iliyopangwa itokee bahati mbaya mwanakikundi awe na safari, amefiwa, au kuumwa.  Lakini kama unajitambua unaweza kutenga dakika 45 kila siku iliyopangwa ili kuhudhuria vikao.
 
"Wote tuna majukumu lakini kama yako yamezidi basi hufai kuwa katika kikundi"

2 comments:

  1. ""Ukiona mtu ana udhuru katika kikundi basi ujue huyo hajitambui na hatakuja kufanikiwa hata iweje""
    Ndugu Buberwa napenda kukufahamisha kwamba kama wewe ni kiongozi katika chama inabidi uwe unatafuta maneno ya busara yakuongea na wanachama wako kwa kipindi huaika. Kusema kwamba "MTU HATAFANIKIWA HATA IWEJE KWA SABABU Ana HUDHURU" Huko ni kukosa busara tena wanachama wako wataona kama unalazimisha Vitu kwa manufaa yako Mwenyewe. Ina maana wewe hujawahi kupatwa na Udhuru? Hujawahi kuumwa? hujawahi kufiwa? Haya ni mambo ya kujiuliza kabla haujaingia kwenye mitandao na kuandika upuuzi wako maana wewe si Mungu kwamba kila unalopanga linafanikiwa.
    Ukitaka kuona kwamba wewe si Mungu mtu hao wanachama wako wenyewe hawauzurii vikao, hii ni kuonyesha kwamba kila jambo linawezekana katika uliwwengu huu, Laiti kama ungelikuwa ni Mungu hakuna ambalo lingeshindikana, Hivyo basi kuwa na busara kama mtu mzima, sio kukaa na kutukana watu kama sio kuwakashifu kwa mapungufu yao ya kiuchumi.
    Yangu ni hayo. 0713-185-183

    ReplyDelete
  2. Nashukuru Sana kwa ushauri wako Gerald Mvella, ni vyema umeonesha Jinsi gani umekasirishwa na matumizi ya lugha. Barikiwa

    ReplyDelete